Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 23:1-9

Mithali 23:1-9 NENO

Uketipo kula chakula na mtawala, angalia vyema kile kilicho mbele yako, na utie kisu kooni mwako kama ukiwa mlafi. Usitamani vyakula vyake vitamu kwa kuwa chakula hicho ni cha hila. Usijitaabishe ili kuupata utajiri, uwe na hekima kuonesha kujizuia. Kufumba na kufumbua utajiri hutoweka, huwa kama umepata mabawa ghafula, ukaruka na kutoweka angani kama tai. Usile chakula cha mtu mchoyo, usitamani vyakula vyake vitamu, kwa maana yeye ni aina ya mtu ambaye kila mara anafikiri kuhusu gharama. Anakuambia, “Kula na kunywa,” lakini moyo wake hauko pamoja nawe. Utatapika kile kidogo ulichokula, nawe utakuwa umepoteza bure maneno yako ya kumsifu. Usizungumze na mpumbavu, kwa maana atadhihaki hekima ya maneno yako.