Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 2:1-10

Mit 2:1-10 SUV

Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu; Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu; Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika; Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, Na kupata kumjua Mungu. Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu; Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili; Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu; Apate kuyalinda mapito ya hukumu, Na kuhifadhi njia ya watakatifu wake. Ndipo utakapofahamu haki na hukumu, Na adili, na kila njia njema. Maana hekima itaingia moyoni mwako, Na maarifa yatakupendeza nafsi yako

Soma Mit 2

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha