Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Lk 3

3
Tangazo la Yohana
1Mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alipokuwa liwali wa Uyahudi, na Herode mfalme wa Galilaya, na Filipo, ndugu yake, mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania mfalme wa Abilene, 2wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa, neno la Mungu lilimfikia Yohana, mwana wa Zakaria, jangwani. 3#Mt 3:1-12; Mk 1:1-8Akafika nchi yote iliyo karibu na Yordani, akihubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi, 4#Isa 40:3-5kama ilivyoandikwa katika chuo cha maneno ya nabii Isaya;
Sauti ya mtu aliaye nyikani,
Itengenezeni njia ya Bwana,
Yanyosheni mapito yake.
5Kila bonde litajazwa,
Na kila mlima na kilima kitashushwa;
Palipopotoka patakuwa pamenyoka,
Na palipoparuza patalainishwa;
6 # Mdo 28:28 Na wote wenye mwili watauona wokovu wa Mungu.
7 # Mt 12:34; 23:33; Yn 3:36 Basi, aliwaambia makutano ya wale waliomwendea ili awabatize, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? 8#Yn 8:33Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto. 9#Mt 7:19Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni. 10Makutano wakamwuliza, Tufanye nini basi? 11Akawajibu akiwaambia, Mwenye kanzu mbili na ampe asiye na kanzu; na mwenye vyakula na afanye vivyo hivyo. 12#Lk 7:29Watoza ushuru nao wakaja kubatizwa, wakamwuliza, Mwalimu, tufanye nini sisi? 13Akawaambia, Msitoze kitu zaidi kuliko mlivyoamriwa. 14Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtoshewe na mshahara wenu.
15 # Yn 1:19-28 Basi, watu walipokuwa wakingoja yatakayotokea, wote wakiwaza-waza mioyoni mwao habari za Yohana, kama labda yeye ndiye Kristo, 16#Mdo 13:25Yohana alijibu akawaambia wote, Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto; 17ambaye pepeo lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake, na kuikusanya ngano ghalani mwake, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
18Basi, kwa maonyo mengine mengi aliwahubiri watu. 19#Mt 14:3-4; Mk 6:17-18Lakini mfalme Herode alipokaripiwa na yeye kwa ajili ya Herodia, mke wa nduguye, na maovu yote aliyoyafanya Herode, 20aliongeza na hili juu ya yote, alimfunga Yohana gerezani.
Kubatizwa kwa Yesu
21 # Mt 3:13-17; Mk 1:9-11; Yn 1:32 Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka; 22#Mwa 22:2; Zab 2:7; Isa 42:1; Mt 3:17; Mk 1:11; Lk 9:35Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.
Ukoo wa Yesu
23 # Mt 1:1-17 # Lk 4:22 Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli, 24wa Mathati, wa Lawi, wa Melki, wa Yana, wa Yusufu, 25wa Matathia, wa Amosi, wa Nahumu, wa Esli, wa Nagai, 26wa Maathi, wa Matathia, wa Semei, wa Yusufu, wa Yuda, 27#1 Nya 3:17; Ezr 3:2wa Yoana, wa Resa, wa Zerubabeli, wa Shealtieli, wa Neri, 28wa Melki, wa Adi, wa Kosamu, wa Elmadamu, wa Eri, 29wa Yoshua, wa Eliezeri, wa Yorimu, wa Mathati, wa Lawi, 30wa Simeoni, wa Yuda, wa Yusufu, wa Yonamu, wa Eliakimu, 31#1 Sam 16:1,13; 2 Sam 5:14wa Melea, wa Mena, wa Matatha, wa Nathani, wa Daudi, 32#Rut 4:22wa Yese, wa Obedi, wa Boazi, wa Salmoni, wa Nashoni, 33#1 Nya 2:1-5; Mwa 29:35wa Aminadabu, wa Aramu, wa Hesroni, wa Peresi, wa Yuda, 34#Mwa 21:2,3; 11:10-26; 1 Nya 1:24-27wa Yakobo, wa Isaka, wa Ibrahimu, wa Tera, wa Nahori, 35wa Serugi, wa Ragau, wa Pelegi, wa Eberi, wa Sala, 36#Mwa 5:3-32; 1 Nya 1:1-4; Mwa 4:25; 11:10wa Kenani, wa Arfaksadi, wa Shemu, wa Nuhu, wa Lameki, 37wa Methusela, wa Henoko, wa Yaredi, wa Mahalaleli, wa Kenani, 38#Mwa 5:1-3wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu, wa Mungu.

Iliyochaguliwa sasa

Lk 3: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha