Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yos 15:20-63

Yos 15:20-63 SUV

Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Yuda sawasawa na jamaa zao. Miji ya mwisho ya kabila ya wana wa Yuda upande wa kuelekea mpaka wa Edomu katika nchi ya Negebu ilikuwa ni Kabseeli, na Ederi, na Yaguri; na Kina, na Dimona, na Adada; na Kedeshi, na Hazori, na Ithnani; na Zifu, na Telemu, na Bealothi; na Hazor-hadata, na Kerioth-hezroni (ndio Hazori); na Amamu, na Shema, na Molada; na Hasar-gada, na Heshmoni, na Bethpeleti; na Hasarshuali, na Beer-sheba, na Biziothia; na Baala, na Iyimu, na Esemu; na Eltoladi, na Kesili, na Horma; na Siklagi, na Madmana, na Sansana; na Lebaothi, na Shilhimu, na Aini, na Rimoni; miji hiyo yote ni miji ishirini na kenda, pamoja na vijiji vyake. Katika nchi ya Shefela, Eshtaoli, na Sora, na Ashna, na Zanoa, na Enganimu, na Tapua, na Enamu; na Yarmuthi, na Adulamu, na Soko, na Azeka; na Shaarimu, na Adithaimu, na Gedera, na Gederothaimu miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake. Senani, na Hadasha, na Migdal-gadi; na Dilani, na Mispe, na Yoktheeli; na Lakishi, na Boskathi, na Egloni; na Kaboni, na Lamasi, na Kithilishi; na Gederothi, na Beth-dagoni, na Naama, na Makeda; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake. Libna, na Etheri, na Ashani; na Yifta, na Ashna, na Nesibu; na Keila, na Akizibu, na Maresha; miji kenda, pamoja na vijiji vyake. Ekroni, pamoja na miji yake na vijiji vyake; kutoka huko Ekroni mpaka baharini, yote iliyokuwa upande wa Ashdodi, pamoja na vijiji vyake. Ashdodi, na miji yake na vijiji vyake; na Gaza, na miji yake na vijiji vyake; mpaka kijito cha Misri, na bahari kubwa, na mpaka wake. Na katika nchi ya vilima, Shamiri, na Yatiri, na Soko; na Dana, na Kiriath-sana (ambao ni Debiri); na Anabu, na Eshtemoa, na Animu; na Gosheni, na Holoni, na Gilo; miji kumi na mmoja, pamoja na vijiji vyake. Arabu, na Duma, na Eshani; na Yanumu, na Beth-tapua, na Afeka; na Humta, na Kiriath-arba (ndio Hebroni), na Siori; miji kenda, pamoja na vijiji vyake. Maoni, na Karmeli, na Zifu, na Yuta; na Yezreeli, na Yokdeamu, na Zanoa; na Kaini, na Gibea, na Timna; miji kumi, pamoja na vijiji vyake. Halhuli, na Bethsuri, na Gedori; na Maarathi, na Bethanothi, Eltekoni; miji sita, pamoja na vijiji vyake. Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu), na Raba; miji miwili, pamoja vijiji vyake. Huko nyikani, Betharaba, na Midini, na Sekaka; na Nibshani, na huo Mji wa Chumvi, na Engedi; miji sita, pamoja na vijiji vyake. Tena katika habari ya Wayebusi, hao wenye kukaa Yerusalemu, wana wa Yuda hawakuweza kuwatoa; lakini hao Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Yuda huko Yerusalemu hata hivi leo.

Soma Yos 15