Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yoshua 15:20-63

Yoshua 15:20-63 Biblia Habari Njema (BHN)

Hii ndiyo nchi waliyopewa watu wa kabila la Yuda kulingana na koo zake. Miji iliyokuwa upande wa kusini kabisa wa nchi ya Yuda kuelekea mpaka wa Edomu ilikuwa: Kabseeli, Ederi, Yaguri, Kina, Dimona, Adada, Kedeshi, Hazori, Ithnani, Zifu, Telemu, Bealothi, Hazor-hadata, Kerioth-hezroni (yaani Hazori), Amamu, Shema, Molada, Hasar-gada, Heshmoni, Beth-peleti, Hasar-shuali, Beer-sheba, Biziothia, Baala, Iyimu, Ezemu, Eltoladi, Kesili, Horma, Siklagi, Madmana, Sansana, Lebaothi, Shilhimu, Aini na Rimoni. Jumla ya miji waliyopewa ni ishirini na tisa pamoja na vijiji vyake. Miji iliyokuwa kwenye tambarare ilikuwa: Eshtaoli, Sora, Ashna, Zanoa, Enganimu, Tapua, Enamu, Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka, Shaaraimu, Adithaimu, Gedera na Gederothaimu. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na minne pamoja na vijiji vyake. Walipewa pia miji ya Senani, Hadasha, Migdal-gadi, Dileani, Mizpa, Yoktheeli, Lakishi, Boskathi, Egloni, Kaboni, Lahmamu, Kithlishi, Gederothi, Beth-dagoni, Naama na Makeda. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na sita pamoja na vijiji vyake. Tena walipewa miji ya Libna, Etheri, Ashani, Yifta, Ashna, Nezibu, Keila, Akzibu na Maresha. Jumla ya miji waliyopewa ni tisa pamoja na vijiji vyake. Vilevile walipewa Ekroni pamoja na miji yake midogo na vijiji, miji yote na vijiji vilivyokuwa karibu na Ashdodi kati ya Ekroni na bahari, Ashdodi na Gaza pamoja na miji na vijiji vyake, mpaka kijito cha Misri hadi pwani ya bahari ya Mediteranea. Miji iliyokuwa kwenye eneo la milimani ni Shamiri, Yatiri, Soko, Dana, Kiriath-sana (yaani Debiri), Anabu, Eshtemoa, Animu, Gosheni, Holoni na Gilo. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na mmoja pamoja na vijiji vyake. Walipewa pia miji ya Arabu, Duma, Eshani, Yanimu, Beth-tapua, Afeka, Humta, Kiriath-arba (yaani Hebroni) na Siori. Jumla ya miji waliyopewa ni tisa pamoja na vijiji vyake. Pia walipewa miji ya Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta, Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa, Kaini, Gibea na Timna. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi pamoja na vijiji vyake. Vilevile miji ya Halhuli, Beth-suri, Gedori, Maarathi, Beth-anothi na Eltekoni. Jumla ya miji waliyopewa ni sita pamoja na vijiji vyake. Kadhalika walipewa Kiriath-baali, uitwao pia Kiriath-yearimu, na Raba. Jumla ya miji waliyopewa ni miwili pamoja na vijiji vyake. Miji ya nyikani ilikuwa Beth-araba, Midini, Sekaka, Nibshani, Mji wa Chumvi na Engedi. Jumla ya miji waliyopewa ni sita pamoja na vijiji vyake. Lakini watu wa Yuda hawakuweza kuwafukuza Wayebusi, ambao ndio waliokuwa wenyeji wa Yerusalemu, na mpaka leo Wayebusi bado wanaishi mjini humo pamoja na watu wa Yuda.

Shirikisha
Soma Yoshua 15

Yoshua 15:20-63 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Yuda sawasawa na jamaa zao. Miji ya mwisho ya kabila la wana wa Yuda upande wa kuelekea mpaka wa Edomu katika nchi ya Negebu ilikuwa ni Kabseeli, Ederi, Yaguri; Kina, Dimona, Adada; Kedeshi, Hazori, Ithnani; Zifu, Telemu, Bealothi; Hazor-hadata, Kerioth-hezroni (ndio Hazori); Amamu, Shema, Molada; Hasar-gada, Heshmoni, Beth-peleti; Hasar-shuali, Beer-sheba, Biziothia; Baala, Iyimu, Esemu; Eltoladi, Kesili, Horma; Siklagi, Madmana, Sansana; Lebaothi, Shilhimu, Aini na Rimoni; miji hiyo yote ni miji ishirini na tisa, pamoja na vijiji vyake. Katika nchi ya Shefela, Eshtaoli, Sora, Ashna, Zanoa, Enganimu, Tapua, Enamu; Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka; Shaarimu, Adithaimu, Gedera na Gederothaimu miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake. Senani, Hadasha, Migdal-gadi; Dilani, Mispe, Yoktheeli; Lakishi, Bozkathi, Egloni; Kaboni, Lamasi, Kithilishi; Gederothi, Beth-dagoni, Naama na Makeda; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake. Libna, Etheri, Ashani; Yifta, Ashna, Nesibu; Keila, Akizibu na Maresha; miji tisa, pamoja na vijiji vyake. Ekroni, pamoja na miji yake na vijiji vyake; kutoka huko Ekroni mpaka baharini, yote iliyokuwa upande wa Ashdodi, pamoja na vijiji vyake. Ashdodi, na miji yake na vijiji vyake; Gaza, na miji yake na vijiji vyake; mpaka kijito cha Misri, na bahari kuu na pwani yake. Na katika nchi ya vilima, Shamiri, Yatiri, Soko; Dana, Kiriath-sana (ambao ni Debiri); Anabu, Eshtemoa, Animu; Gosheni, Holoni na Gilo; miji kumi na mmoja, pamoja na vijiji vyake. Arabu, Duma, Eshani; Yanumu, Beth-tapua, Afeka; Humta, Kiriath-arba (ndio Hebroni) na Siori; miji tisa, pamoja na vijiji vyake. Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta; Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa; Kaini, Gibea na Timna; miji kumi, pamoja na vijiji vyake. Halhuli, Beth-suri, Gedori; Maarathi, Bethanothi na Eltekoni; miji sita, pamoja na vijiji vyake. Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu) na Raba; miji miwili, pamoja vijiji vyake. Huko nyikani, Beth-araba, na Midini, na Sekaka; na Nibshani, na huo Mji wa Chumvi, na Engedi; miji sita, pamoja na vijiji vyake. Tena katika habari ya Wayebusi, hao wenye kukaa Yerusalemu, wana wa Yuda hawakuweza kuwatoa; lakini hao Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Yuda huko Yerusalemu hata hivi leo.

Shirikisha
Soma Yoshua 15

Yoshua 15:20-63 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Yuda sawasawa na jamaa zao. Miji ya mwisho ya kabila ya wana wa Yuda upande wa kuelekea mpaka wa Edomu katika nchi ya Negebu ilikuwa ni Kabseeli, na Ederi, na Yaguri; na Kina, na Dimona, na Adada; na Kedeshi, na Hazori, na Ithnani; na Zifu, na Telemu, na Bealothi; na Hazor-hadata, na Kerioth-hezroni (ndio Hazori); na Amamu, na Shema, na Molada; na Hasar-gada, na Heshmoni, na Bethpeleti; na Hasarshuali, na Beer-sheba, na Biziothia; na Baala, na Iyimu, na Esemu; na Eltoladi, na Kesili, na Horma; na Siklagi, na Madmana, na Sansana; na Lebaothi, na Shilhimu, na Aini, na Rimoni; miji hiyo yote ni miji ishirini na kenda, pamoja na vijiji vyake. Katika nchi ya Shefela, Eshtaoli, na Sora, na Ashna, na Zanoa, na Enganimu, na Tapua, na Enamu; na Yarmuthi, na Adulamu, na Soko, na Azeka; na Shaarimu, na Adithaimu, na Gedera, na Gederothaimu miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake. Senani, na Hadasha, na Migdal-gadi; na Dilani, na Mispe, na Yoktheeli; na Lakishi, na Boskathi, na Egloni; na Kaboni, na Lamasi, na Kithilishi; na Gederothi, na Beth-dagoni, na Naama, na Makeda; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake. Libna, na Etheri, na Ashani; na Yifta, na Ashna, na Nesibu; na Keila, na Akizibu, na Maresha; miji kenda, pamoja na vijiji vyake. Ekroni, pamoja na miji yake na vijiji vyake; kutoka huko Ekroni mpaka baharini, yote iliyokuwa upande wa Ashdodi, pamoja na vijiji vyake. Ashdodi, na miji yake na vijiji vyake; na Gaza, na miji yake na vijiji vyake; mpaka kijito cha Misri, na bahari kubwa, na mpaka wake. Na katika nchi ya vilima, Shamiri, na Yatiri, na Soko; na Dana, na Kiriath-sana (ambao ni Debiri); na Anabu, na Eshtemoa, na Animu; na Gosheni, na Holoni, na Gilo; miji kumi na mmoja, pamoja na vijiji vyake. Arabu, na Duma, na Eshani; na Yanumu, na Beth-tapua, na Afeka; na Humta, na Kiriath-arba (ndio Hebroni), na Siori; miji kenda, pamoja na vijiji vyake. Maoni, na Karmeli, na Zifu, na Yuta; na Yezreeli, na Yokdeamu, na Zanoa; na Kaini, na Gibea, na Timna; miji kumi, pamoja na vijiji vyake. Halhuli, na Bethsuri, na Gedori; na Maarathi, na Bethanothi, Eltekoni; miji sita, pamoja na vijiji vyake. Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu), na Raba; miji miwili, pamoja vijiji vyake. Huko nyikani, Betharaba, na Midini, na Sekaka; na Nibshani, na huo Mji wa Chumvi, na Engedi; miji sita, pamoja na vijiji vyake. Tena katika habari ya Wayebusi, hao wenye kukaa Yerusalemu, wana wa Yuda hawakuweza kuwatoa; lakini hao Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Yuda huko Yerusalemu hata hivi leo.

Shirikisha
Soma Yoshua 15

Yoshua 15:20-63 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Huu ndio urithi wa kabila la Yuda, kufuatana na koo zao: Miji ya kusini kabisa ya kabila la Yuda katika Negebu kuelekea mpaka wa Edomu ilikuwa: Kabseeli, Ederi, Yaguri, Kina, Dimona, Adada, Kedeshi, Hazori, Ithnani, Zifu, Telemu, Bealothi, Hazor-Hadata, Kerioth-Hezroni (yaani Hazori), Amamu, Shema, Molada, Hasar-Gada, Heshmoni, Beth-Peleti, Hasar-Shuali, Beer-Sheba, Biziothia, Baala, Iyimu, Esemu, Eltoladi, Kesili, Horma, Siklagi, Madmana, Sansana, Lebaothi, Shilhimu, Aini na Rimoni; hiyo yote ni miji ishirini na tisa, pamoja na vijiji vyake. Katika Shefela: Eshtaoli, Sora, Ashna, Zanoa, En-Ganimu, Tapua, Enamu, Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka, Shaaraimu, Adithaimu na Gedera (au Gederothaimu); yote ni miji kumi na nne, pamoja na vijiji vyake. Senani, Hadasha, Migdal-Gadi, Dileani, Mispa, Yoktheeli, Lakishi, Boskathi, Egloni, Kaboni, Lamasi, Kitlishi, Gederothi, Beth-Dagoni, Naama na Makeda; yote ni miji kumi na sita pamoja na vijiji vyake. Libna, Etheri, Ashani, Yifta, Ashna, Nesibu, Keila, Akzibu na Maresha; yote ni miji tisa pamoja na vijiji vyake. Ekroni, pamoja na makazi yake na vijiji vyake; magharibi mwa Ekroni, maeneo yote yaliyokuwa karibu na Ashdodi, pamoja na vijiji vyake; Ashdodi, makazi yake na vijiji vyake, na Gaza, makazi yake na vijiji vyake, hadi kufikia Kijito cha Misri na Pwani ya Bahari Kuu. Katika nchi ya vilima: Shamiri, Yatiri, Soko, Dana, Kiriath-Sana (yaani Debiri), Anabu, Eshtemoa, Animu, Gosheni, Holoni na Gilo; miji kumi na moja pamoja na vijiji vyake. Arabu, Duma, Ashani, Yanimu, Beth-Tapua, Afeka, Humta, Kiriath-Arba (yaani Hebroni), na Siori; miji tisa pamoja na vijiji vyake. Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta, Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa, Kaini, Gibea na Timna; miji kumi pamoja na vijiji vyake. Halhuli, Beth-Suri, Gedori, Maarathi, Beth-Anothi na Eltekoni; miji sita pamoja na vijiji vyake. Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu) na Raba; miji miwili pamoja na vijiji vyake. Huko jangwani: Beth-Araba, Midini, Sekaka, Nibshani, Mji wa Chumvi, na En-Gedi; miji sita pamoja na vijiji vyake. Yuda hakuweza kuwafukuza Wayebusi, walioishi Yerusalemu; hadi leo Wayebusi huishi huko pamoja na watu wa Yuda.

Shirikisha
Soma Yoshua 15