Ayu 8:3-6
Ayu 8:3-6 SUV
Je! Mungu hupotosha hukumu? Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki? Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi, Naye amewatia mkononi mwa kosa lao; Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi; Ukiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa.