Yobu 8:3-6
Yobu 8:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwani, wadhani Mungu hupotosha haki? Au, je, Mungu Mwenye Nguvu hupotosha ukweli? Kama watoto wako wamemkosea Mungu, yeye amewalipiza matokeo ya uhalifu wao. Kama utamtafuta Mungu ukamsihi huyo Mungu mwenye nguvu, kama wewe u safi moyoni na mnyofu, kweli Mungu atakuja kukusaidia, na kukujalia makao unayostahili.
Yobu 8:3-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Je! Mungu hupotosha hukumu? Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki? Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi, Naye amewatia mkononi mwa kosa lao; Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi; Ikiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa.
Yobu 8:3-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Je! Mungu hupotosha hukumu? Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki? Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi, Naye amewatia mkononi mwa kosa lao; Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi; Ukiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa.
Yobu 8:3-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Je, Mungu hupotosha hukumu? Je, Mwenyezi hupotosha kile kilicho haki? Watoto wako walipomtenda dhambi, aliwapa adhabu ya dhambi yao. Lakini ukimtafuta Mungu, nawe ukamsihi Mwenyezi, ikiwa wewe ni safi na mnyofu, hata sasa atainuka mwenyewe kwa niaba yako, na kukurudisha katika mahali pako pa haki.