Ayu 38:1-4
Ayu 38:1-4 SUV
Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema, Ni nani huyu atiaye mashauri giza Kwa maneno yasiyo na maarifa? Basi jifunge viuno kama mwanamume, Maana nitakuuliza neno, nawe niambie. Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu.