Yobu 38:1-4
Yobu 38:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Hapo Mwenyezi-Mungu alimjibu Yobu kutoka dhoruba: “Nani wewe unayevuruga mashauri yangu kwa maneno yasiyo na akili? Jikaze kama mwanamume, nami nitakuuliza nawe utanijibu. “Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya dunia? Niambie, kama una maarifa.
Yobu 38:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema, Ni nani huyu atiaye ushauri giza Kwa maneno yasiyo na maarifa? Basi jifunge viuno kama mwanamume, Maana nitakuuliza neno, nawe niambie. Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama una ufahamu.
Yobu 38:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema, Ni nani huyu atiaye mashauri giza Kwa maneno yasiyo na maarifa? Basi jifunge viuno kama mwanamume, Maana nitakuuliza neno, nawe niambie. Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu.
Yobu 38:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kisha BWANA akamjibu Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli. Akasema: “Nani huyu atiaye mashauri yangu giza kwa maneno yasiyo na maarifa? Jikaze kama mwanaume; nitakuuliza swali, nawe unijibu. “Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia? Niambie, kama unafahamu.