Ayu 13:15-18
Ayu 13:15-18 SUV
Tazama, ataniua; sina tumaini; Ila hata hivyo nitaithibitisha njia yangu mbele yake. Hili nalo litakuwa ni wokovu wangu; Kwani asiyemcha Mungu hatakaribia mbele yake. Sikieni sana maneno yangu, Maelezo yangu na yaingie masikioni mwenu. Angalieni sasa, nimekwisha kulitengeneza neno langu, Najua ya kuwa ni mwenye haki mimi.