Yobu 13:15-18
Yobu 13:15-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu aniue akitaka, sina la kupoteza, hata hivyo nitautetea mwenendo wangu mbele yake. Kama nikifaulu hapo nitakuwa nimeshinda, maana mtu mwovu hawezi kwenda mbele yake. Sikilizeni kwa makini maneno yangu, maelezo yangu na yatue masikioni mwenu. Kesi yangu nimeiandaa vilivyo, nina hakika mimi sina hatia.
Yobu 13:15-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tazama, ataniua; sina tumaini; Ila hata hivyo nitaithibitisha njia yangu mbele yake. Hili nalo litakuwa ni wokovu wangu; Kwani asiyemcha Mungu hatakaribia mbele yake. Sikieni sana maneno yangu, Maelezo yangu na yaingie masikioni mwenu. Angalieni sasa, nimekwisha kulitengeneza neno langu, Najua ya kuwa mimi ni mwenye haki.
Yobu 13:15-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tazama, ataniua; sina tumaini; Ila hata hivyo nitaithibitisha njia yangu mbele yake. Hili nalo litakuwa ni wokovu wangu; Kwani asiyemcha Mungu hatakaribia mbele yake. Sikieni sana maneno yangu, Maelezo yangu na yaingie masikioni mwenu. Angalieni sasa, nimekwisha kulitengeneza neno langu, Najua ya kuwa ni mwenye haki mimi.
Yobu 13:15-18 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ingawa ataniua, bado nitamtumaini; hakika nitazitetea njia zangu mbele zake. Naam, hili litanigeukia kuwa wokovu wangu, kwa maana hakuna mtu asiyemcha Mungu atakayethubutu kuja mbele yake! Sikilizeni maneno yangu kwa makini; nayo masikio yenu yaingize kile nisemacho. Sasa kwa kuwa nimekwisha tayarisha kesi yangu, ninajua nitahesabiwa kuwa haki.