Ayu 12:7-10
Ayu 12:7-10 SUV
Lakini sasa waulize hao wanyama, nao watakufundisha; Na nyuni wa angani, nao watakuambia; Au nena na nchi, nayo itakufundisha; Nao samaki wa baharini watakutangazia. Katika hawa wote ni yupi asiyejua, Kwamba ni mkono wa BWANA uliofanya haya? Ambaye nafsi ya kila kilicho hai i mkononi mwake, Na pumzi zao wanadamu wote.