Yobu 12:7-10
Yobu 12:7-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini waulize wanyama nao watakufunza; waulize ndege nao watakuambia. Au iulize mimea nayo itakufundisha; sema na samaki nao watakuarifu. Nani kati ya viumbe hivyo, asiyejua kwamba Mwenyezi-Mungu ametenda hayo? Uhai wa kila kiumbe hai umo mikononi mwake; kadhalika na pumzi ya uhai wa binadamu.
Yobu 12:7-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini sasa waulize hao wanyama, nao watakufundisha; Na ndege wa angani, nao watakuambia; Au nena na nchi, nayo itakufundisha; Nao samaki wa baharini watakutangazia. Katika hawa wote ni yupi asiyejua, Kwamba ni mkono wa BWANA uliofanya haya? Ambaye nafsi ya kila kilicho hai i mkononi mwake, Na pumzi zao wanadamu wote.
Yobu 12:7-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini sasa waulize hao wanyama, nao watakufundisha; Na nyuni wa angani, nao watakuambia; Au nena na nchi, nayo itakufundisha; Nao samaki wa baharini watakutangazia. Katika hawa wote ni yupi asiyejua, Kwamba ni mkono wa BWANA uliofanya haya? Ambaye nafsi ya kila kilicho hai i mkononi mwake, Na pumzi zao wanadamu wote.
Yobu 12:7-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Lakini ulizeni wanyama, nao watawafundisha, au ndege wa angani, nao watawaambia; au zungumzeni na dunia, nayo itawafundisha, au acheni samaki wa baharini wawape taarifa. Ni nani miongoni mwa hawa wote asiyejua kwamba mkono wa BWANA ndio uliofanya hili? Mkononi mwake kuna uhai wa kila kiumbe, na pumzi ya wanadamu wote.