Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 75:1-10

Zaburi 75:1-10 NEN

Ee Mungu, tunakushukuru, tunakushukuru wewe, kwa kuwa jina lako li karibu; watu husimulia matendo yako ya ajabu. Unasema, “Ninachagua wakati maalum; ni mimi nihukumuye kwa haki. Wakati dunia na watu wake wote inapotetemeka, ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara. Kwa wale wenye majivuno ninasema, ‘Msijisifu tena,’ kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu. Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu; msiseme kwa shingo zilizonyooshwa.’ ” Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibi au kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu. Bali Mungu ndiye ahukumuye: Humshusha huyu na kumkweza mwingine. Mkononi mwa BWANA kuna kikombe kilichojaa mvinyo unaotoka povu uliochanganywa na vikolezo; huumimina, nao waovu wote wa dunia hunywa mpaka tone la mwisho. Bali mimi, nitatangaza hili milele; nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo. Nitazikatilia mbali pembe za waovu wote, bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu.

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha