Zaburi 116:12-19
Zaburi 116:12-19 NENO
Nimrudishie BWANA nini kwa wema wake wote alionitendea? Nitakiinua kikombe cha wokovu na kulitangaza jina la BWANA. Nitazitimiza nadhiri zangu kwa BWANA mbele za watu wake wote. Kifo cha watakatifu kina thamani machoni pa BWANA. Ee BWANA, hakika mimi ni mtumishi wako, mimi ni mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako; umeniweka huru toka katika minyororo yangu. Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru na kuliita jina la BWANA. Nitazitimiza nadhiri zangu kwa BWANA mbele za watu wake wote, katika nyua za nyumba ya BWANA, katikati yako, ee Yerusalemu.