Zaburi 116:12-19
Zaburi 116:12-19 Biblia Habari Njema (BHN)
Nimrudishie nini Mwenyezi-Mungu, kwa ukarimu wote alionitendea? Nitamtolea tambiko ya divai kwa kunikomboa, nitaomba kwa jina lake Mwenyezi-Mungu. Nitamtimizia Mwenyezi-Mungu nadhiri zangu, mbele ya watu wake wote. Kifo cha waaminifu wake Mwenyezi-Mungu si jambo dogo mbele yake. Ee Mwenyezi-Mungu, mimi ni mtumishi wako; ni mtumishi wako, mtoto wa mjakazi wako; umenifungulia vifungo vyangu. Nitakutolea tambiko za shukrani, na kukupa heshima zangu. Nitakutimizia ahadi zangu, ee Mwenyezi-Mungu mbele ya watu wako wote, waliokusanyika hekaluni mwako, katikati ya Yerusalemu. Msifuni Mwenyezi-Mungu!
Zaburi 116:12-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nimrudishie BWANA nini Kwa ukarimu wake wote alionitendea? Nitakipokea kikombe cha wokovu; Na kulitangaza jina la BWANA; Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA, Naam, mbele ya watu wake wote. Kifo cha waaminifu wa Mungu, kina thamani machoni pa BWANA. Ee BWANA, hakika mimi ni mtumishi wako, Mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako, Umevifungua vifungo vyangu. Nitakutolea dhabihu ya kushukuru; Na kulitangaza jina la BWANA; Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA, Naam, mbele ya watu wake wote. Katika nyua za nyumba ya BWANA, Ndani yako, Ee Yerusalemu.
Zaburi 116:12-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nimrudishie BWANA nini Kwa ukarimu wake wote alionitendea? Nitakipokea kikombe cha wokovu; Na kulitangaza jina la BWANA; Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA, Naam, mbele ya watu wake wote. Ina thamani machoni pa BWANA Mauti ya wacha Mungu wake. Ee BWANA, hakika mimi ni mtumishi wako, Mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako, Umevifungua vifungo vyangu. Nitakutolea dhabihu ya kushukuru; Na kulitangaza jina la BWANA; Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA, Naam, mbele ya watu wake wote. Katika nyua za nyumba ya BWANA, Ndani yako, Ee Yerusalemu.
Zaburi 116:12-19 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nimrudishie BWANA nini kwa wema wake wote alionitendea? Nitakiinua kikombe cha wokovu na kulitangaza jina la BWANA. Nitazitimiza nadhiri zangu kwa BWANA mbele za watu wake wote. Kifo cha watakatifu kina thamani machoni pa BWANA. Ee BWANA, hakika mimi ni mtumishi wako, mimi ni mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako; umeniweka huru toka katika minyororo yangu. Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru na kuliita jina la BWANA. Nitazitimiza nadhiri zangu kwa BWANA mbele za watu wake wote, katika nyua za nyumba ya BWANA, katikati yako, ee Yerusalemu.