Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 115

115
Zaburi 115
Mungu Mmoja wa kweli
1Sio kwetu sisi, Ee Bwana, sio kwetu sisi,
bali utukufu ni kwa jina lako,
kwa sababu ya upendo
na uaminifu wako.
2Kwa nini mataifa waseme,
“Yuko wapi Mungu wao?”
3Mungu wetu yuko mbinguni,
naye hufanya lolote limpendezalo.
4Lakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu,
zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
5Zina vinywa, lakini haziwezi kusema,
zina macho, lakini haziwezi kuona;
6zina masikio, lakini haziwezi kusikia,
zina pua, lakini haziwezi kunusa;
7zina mikono, lakini haziwezi kupapasa,
zina miguu, lakini haziwezi kutembea;
wala koo zao haziwezi kutoa sauti.
8Wale wanaozitengeneza watafanana nazo,
vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.
9Ee nyumba ya Israeli, mtumainini Bwana,
yeye ni msaada na ngao yao.
10Ee nyumba ya Haruni, mtumainini Bwana,
yeye ni msaada na ngao yao.
11Ninyi mnaomcha, mtumainini Bwana,
yeye ni msaada na ngao yao.
12 Bwana anatukumbuka na atatubariki:
ataibariki nyumba ya Israeli,
ataibariki nyumba ya Haruni,
13atawabariki wale wanaomcha Bwana,
wadogo kwa wakubwa.
14 Bwana na awawezeshe kuongezeka,
ninyi na watoto wenu.
15Mbarikiwe na Bwana
Muumba wa mbingu na dunia.
16Mbingu zilizo juu sana ni mali ya Bwana,
lakini dunia amempa mwanadamu.
17Sio wafu wanaomsifu Bwana,
wale wanaoshuka mahali pa kimya#115:17 mahali pa kimya maana yake Kuzimu; kwa Kiebrania ni Sheol.,
18bali ni sisi tunaomtukuza Bwana,
sasa na hata milele.
Msifuni Bwana.#115:18 Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 115: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia