Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 30:1-4

Mithali 30:1-4 NENO

Misemo ya Aguri mwana wa Yake; usia: Huyu mtu alimwambia Ithieli, naam, kwa Ithieli na Ukali: “Mimi ni mjinga kuliko wanadamu wote; sina ufahamu wa kibinadamu. Sijajifunza hekima, wala sina maarifa ya kumjua yeye Aliye Mtakatifu. Ni nani ameshapanda mbinguni na kushuka? Ni nani ameshakusanya upepo kwenye vitanga vya mikono yake? Ni nani ameshafungia maji kwenye nguo yake? Ni nani ameimarisha miisho yote ya dunia? Jina lake ni nani, na mwanawe anaitwa nani? Niambie kama unajua!