Methali 30:1-4
Methali 30:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Maneno ya Aguri, mwana wa Yake. Mawaidha ambayo mtu huyu alimwambia Ithieli, naam, Ithieli na Ukali. Mimi ni mpumbavu mno, wala si mtu; nayo akili ya binadamu sina. Sijajifunza hekima, wala sijui kitu juu ya Mungu Mtakatifu. Ni nani aliyepanda juu mbinguni akashuka chini? Ni nani aliyekamata upepo mkononi? Ni nani aliyefunga maji katika kitambaa? Ni nani aliyeiweka mipaka yote ya dunia? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe? Niambie kama wajua!
Methali 30:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maneno ya Aguri mwana wa Yake; mausia mtu huyu aliyomwambia Ithieli, naam, Ithieli na Ukali. Hakika nimekuwa kama mnyama, wala si mtu; Wala sina ufahamu wa mwanadamu; Wala sikujifunza hekima; Wala sina maarifa ya kumjua Mtakatifu. Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake? Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua?
Methali 30:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maneno ya Aguri bin Yake; mausia mtu huyu aliyomwambia Ithieli, naam, Ithieli na Ukali. Hakika nimekuwa kama mnyama, wala si mtu; Wala sina ufahamu wa mwanadamu; Wala sikujifunza hekima; Wala sina maarifa ya kumjua Mtakatifu. Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake? Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua?
Methali 30:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Misemo ya Aguri mwana wa Yake; usia: Huyu mtu alimwambia Ithieli, naam, kwa Ithieli na Ukali: “Mimi ni mjinga kuliko wanadamu wote; sina ufahamu wa kibinadamu. Sijajifunza hekima, wala sina maarifa ya kumjua yeye Aliye Mtakatifu. Ni nani ameshapanda mbinguni na kushuka? Ni nani ameshakusanya upepo kwenye vitanga vya mikono yake? Ni nani ameshafungia maji kwenye nguo yake? Ni nani ameimarisha miisho yote ya dunia? Jina lake ni nani, na mwanawe anaitwa nani? Niambie kama unajua!