Mithali 29:9-11
Mithali 29:9-11 NENO
Mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu, mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani. Watu wanaomwaga damu humchukia mtu mwadilifu, na hutafuta kumuua mtu mnyofu. Mpumbavu huonesha hasira yake yote, bali mwenye hekima hujizuia.