Methali 29:9-11
Methali 29:9-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenye hekima akibishana na mpumbavu, mpumbavu huwaka hasira na kucheka bila kutulia. Wapendao kumwaga damu humchukia mtu asiye na hatia, lakini watu wema huyalinda maisha yake. Mpumbavu huonesha hasira yake wazi, lakini mwenye hekima huizuia na kuituliza.
Methali 29:9-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu; Akikasirika au akicheka, pia hapana raha. Wamwagao damu humchukia mtu mkamilifu; Bali wenye haki humtunza nafsi yake. Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote; Bali mwenye hekima huizuia na kuituliza.
Methali 29:9-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu; Akikasirika au akicheka, pia hapana raha. Wamwagao damu humchukia mtu mkamilifu; Bali wenye haki humtunza nafsi yake. Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote; Bali mwenye hekima huizuia na kuituliza.
Methali 29:9-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu, mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani. Watu wanaomwaga damu humchukia mtu mwadilifu, na hutafuta kumuua mtu mnyofu. Mpumbavu huonesha hasira yake yote, bali mwenye hekima hujizuia.