Mithali 29:15-17
Mithali 29:15-17 NENO
Fimbo ya maonyo hutia hekima, bali mtoto asiyeonywa humwaibisha mama yake. Waovu wanapostawi, dhambi huongezeka pia; lakini wenye haki wataliona anguko lao. Mkanye mwanao, naye atakupa amani; atakuletea furaha unayotamani.