Mithali 29:10-18
Mithali 29:10-18 NENO
Watu wanaomwaga damu humchukia mtu mwadilifu, na hutafuta kumuua mtu mnyofu. Mpumbavu huonesha hasira yake yote, bali mwenye hekima hujizuia. Mtawala akisikiliza uongo, maafisa wake wote huwa waovu. Mtu maskini na mtu mdhalimu wanafanana kwa jambo hili: BWANA hutia nuru macho yao wote wawili. Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki, kiti chake kitakuwa thabiti daima. Fimbo ya maonyo hutia hekima, bali mtoto asiyeonywa humwaibisha mama yake. Waovu wanapostawi, dhambi huongezeka pia; lakini wenye haki wataliona anguko lao. Mkanye mwanao, naye atakupa amani; atakuletea furaha unayotamani. Mahali pasipo na ufunuo, watu huacha kujizuia, bali ana heri mtu yule anayeitii sheria.