Methali 29:10-18
Methali 29:10-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Wapendao kumwaga damu humchukia mtu asiye na hatia, lakini watu wema huyalinda maisha yake. Mpumbavu huonesha hasira yake wazi, lakini mwenye hekima huizuia na kuituliza. Mtawala akisikiliza mambo ya uongo, maofisa wake wote watakuwa waovu. Maskini na mkandamizaji wanafanana kwa kitu kimoja: Wote wawili wamepewa macho na Mwenyezi-Mungu. Mfalme anayewaamua maskini kwa haki, atauona utawala wake umeimarika milele. Adhabu na maonyo huleta hekima, lakini mtoto aliyeachwa afanye apendavyo humwaibisha mama yake. Waovu wakitawala maovu huongezeka, lakini waadilifu watashuhudia kuanguka kwao. Mpe nidhamu mwanao naye hatakupa wasiwasi; yeye ataufurahisha moyo wako. Pasipo maono ya kinabii watu hukosa nidhamu; heri mtu yule anayeshika sheria.
Methali 29:10-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wamwagao damu humchukia mtu mkamilifu; Bali wenye haki humtunza nafsi yake. Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote; Bali mwenye hekima huizuia na kuituliza. Mwenye kutawala akisikiliza uongo; Basi watumishi wake wote watakuwa waovu. Maskini na mdhalimu hukutana pamoja; BWANA huwatia nuru macho yao wote wawili. Mfalme awahukumuye maskini kwa uaminifu; Kiti chake cha enzi kitathibitika milele. Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye. Waovu wakiongezeka, maasi huongezeka; Bali wenye haki watayatazama maanguko yao. Mrudi mwanao naye atakustarehesha; Naam, atakufurahisha nafsi yako. Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
Methali 29:10-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Methali 29:10-18 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Watu wanaomwaga damu humchukia mtu mwadilifu, na hutafuta kumuua mtu mnyofu. Mpumbavu huonesha hasira yake yote, bali mwenye hekima hujizuia. Mtawala akisikiliza uongo, maafisa wake wote huwa waovu. Mtu maskini na mtu mdhalimu wanafanana kwa jambo hili: BWANA hutia nuru macho yao wote wawili. Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki, kiti chake kitakuwa thabiti daima. Fimbo ya maonyo hutia hekima, bali mtoto asiyeonywa humwaibisha mama yake. Waovu wanapostawi, dhambi huongezeka pia; lakini wenye haki wataliona anguko lao. Mkanye mwanao, naye atakupa amani; atakuletea furaha unayotamani. Mahali pasipo na ufunuo, watu huacha kujizuia, bali ana heri mtu yule anayeitii sheria.