Mithali 27:15-22
Mithali 27:15-22 NENO
Mke mgomvi ni kama matone yasiyokoma siku ya mvua. Kumzuia ni kama kuuzuia upepo, au kukamata mafuta kwa kiganja cha mkono. Kama vile chuma kinoavyo chuma, ndivyo mtu amnoavyo mwenzake. Yeye autunzaye mtini atakula tunda lake, naye amtunzaye bwana wake ataheshimiwa. Kama uso uonekanavyo kwenye maji, ndivyo hivyo moyo wa mtu humwonesha alivyo. Kuzimu na Uharibifu havishibi, wala macho ya mwanadamu hayashibi. Kalibu husafisha fedha na tanuru husafisha dhahabu, bali mtu hupimwa kwa sifa anazopewa na watu. Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu, ukimtwanga kama nafaka kwa mchi, hutauondoa upumbavu wake.