Methali 27:15-22
Methali 27:15-22 Biblia Habari Njema (BHN)
Mke mgomvi daima, ni sawa na tonatona ya maji siku ya mvua. Kumzuia ni sawa na kuzuia upepo, au kukamata mafuta kwa mkono. Chuma hunoa chuma, kadhalika mtu hufundishwa na wenzake. Anayeutunza mtini hula tini, anayemhudumia bwana wake ataheshimiwa. Kama uso ujionavyo wenyewe majini, ndivyo ujijuavyo mwenyewe moyoni. Kuzimu na Uharibifu kamwe havishibi, kadhalika na macho ya watu hayashibi. Ubora wa fedha au dhahabu hupimwa kwa moto, na mtu hupimwa kutokana na sifa zake. Mtwange mpumbavu katika kinu pamoja na nafaka, lakini hutafaulu kumtenganisha na upumbavu wake.
Methali 27:15-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Matone daima kudondoka siku ya mvua nyingi, Na mwanamke mgomvi ni sawasawa; Atakaye kumzuia huyo huuzuia upepo; Na mkono wake wa kulia hukuta mafuta. Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake. Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake; Naye amhudumiaye bwana wake ataheshimiwa. Kama uso ufananavyo na uso katika maji; Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake. Kuzimu na Uharibifu havishibi; Wala macho ya wanadamu hayashibi. Kalibu ni kwa fedha, na tanuri kwa dhahabu; Na mtu hujaribiwa kwa sifa zake. Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka.
Methali 27:15-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi, Na mwanamke mgomvi ni sawasawa; Atakaye kumzuia huyo huuzuia upepo; Na mkono wake wa kuume hukuta mafuta. Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake. Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake; Naye amhudumiaye bwana wake ataheshimiwa. Kama uso ufananavyo na uso katika maji; Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake. Kuzimu na Uharibifu havishibi; Wala macho ya wanadamu hayashibi. Kalibu ni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu; Na mtu hujaribiwa kwa sifa zake. Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka.
Methali 27:15-22 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mke mgomvi ni kama matone yasiyokoma siku ya mvua. Kumzuia ni kama kuuzuia upepo, au kukamata mafuta kwa kiganja cha mkono. Kama vile chuma kinoavyo chuma, ndivyo mtu amnoavyo mwenzake. Yeye autunzaye mtini atakula tunda lake, naye amtunzaye bwana wake ataheshimiwa. Kama uso uonekanavyo kwenye maji, ndivyo hivyo moyo wa mtu humwonesha alivyo. Kuzimu na Uharibifu havishibi, wala macho ya mwanadamu hayashibi. Kalibu husafisha fedha na tanuru husafisha dhahabu, bali mtu hupimwa kwa sifa anazopewa na watu. Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu, ukimtwanga kama nafaka kwa mchi, hutauondoa upumbavu wake.