Mithali 24:1-4
Mithali 24:1-4 NENO
Usiwaonee wivu watu waovu, usitamani ushirika nao; kwa maana mioyo yao hupanga mambo ya jeuri, nayo midomo yao husema kuhusu kuleta madhara. Kwa hekima nyumba hujengwa, nayo kupitia ufahamu huimarishwa; kwa maarifa vyumba vyake hujazwa vitu vya thamani na vya kupendeza.