Methali 24:1-4
Methali 24:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Usiwaonee wivu watu waovu, wala usitamani kuwa pamoja nao, maana fikira zao zote ni juu ya ukatili, hamna jema lolote litokalo midomoni mwao. Nyumba hujengwa kwa hekima, na kuimarishwa kwa busara. Kwa maarifa vyumba vyake hujazwa vitu vya thamani na vya kupendeza.
Methali 24:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Usiwawaonee wivu watu waovu, Wala usitamani kuwa pamoja nao; Kwa maana moyo wao hufikiri dhuluma, Na midomo yao huongea madhara. Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika, Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza.
Methali 24:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Usiwahusudu watu waovu, Wala usitamani kuwa pamoja nao; Kwa maana moyo wao hufikiri dhuluma, Na midomo yao huongea madhara. Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika, Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza.
Methali 24:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Usiwaonee wivu watu waovu, usitamani ushirika nao; kwa maana mioyo yao hupanga mambo ya jeuri, nayo midomo yao husema kuhusu kuleta madhara. Kwa hekima nyumba hujengwa, nayo kupitia ufahamu huimarishwa; kwa maarifa vyumba vyake hujazwa vitu vya thamani na vya kupendeza.