Mithali 23:10-18
Mithali 23:10-18 NENO
Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani wala kunyemelea kwenye mashamba ya yatima, kwa kuwa Mtetezi wao ni mwenye nguvu, atawatetea dhidi yako. Elekeza moyo wako kwenye mafundisho na masikio yako kwenye maneno ya maarifa. Usimnyime mtoto adhabu, ukimwadhibu kwa fimbo, hatakufa. Mwadhibu kwa fimbo na kuiokoa nafsi yake kutoka mautini. Mwanangu, kama moyo wako una hekima, basi moyo wangu utafurahi, utu wangu wa ndani utafurahi, wakati midomo yako itakapozungumza lililo sawa. Usiuruhusu moyo wako kuwaonea wivu wenye dhambi, bali kila mara uwe na bidii katika kumcha BWANA. Hakika kuna tumaini la baadaye kwa ajili yako, nalo tarajio lako halitakatiliwa mbali.