Methali 23:10-18
Methali 23:10-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Usiondoe alama ya mpaka wa zamani, wala usiingilie mashamba ya yatima, maana Mungu, Mkombozi, ni mwenye nguvu, naye ataitetea haki yao dhidi yako. Tumia akili zako kufuata mafundisho; tumia masikio yako kusikiliza maarifa. Usiache kumrudi mtoto; ukimchapa kiboko hatakufa. Ukimtandika kiboko, utayaokoa maisha yake na kuzimu. Mwanangu, moyo wako ukiwa wenye busara, moyo wangu pia utakuwa wenye furaha. Moyo wangu utashangilia, mdomo wako utakaposema maneno yaliyo sawa. Moyo wako usiwaonee wivu wenye dhambi, ila endelea kumcha Mwenyezi-Mungu siku zote. Hakika kuna kesho ya milele, na tumaini lako halitakuwa bure.
Methali 23:10-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani; Wala usiingie katika mashamba ya yatima; Kwa sababu mkombozi wao ana nguvu; Atawatetea juu yako. Elekeza moyo wako kusikiliza mafundisho; Tega masikio yako kusikia maneno ya maarifa. Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu. Mwanangu, kama moyo wako una hekima, Moyo wangu utafurahi, naam, moyo wangu; Naam, viuno vyangu vitafurahi, Midomo yako inenapo maneno mema. Moyo wako usiwahusudu wenye dhambi; Bali mche BWANA mchana kutwa; Maana bila shaka iko thawabu; Na tumaini lako halitabatilika.
Methali 23:10-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani; Wala usiingie katika mashamba ya yatima; Kwa sababu mkombozi wao ana nguvu; Atawatetea juu yako. Elekeza moyo wako kusikiliza mafundisho; Tega masikio yako kusikia maneno ya maarifa. Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu. Mwanangu, kama moyo wako una hekima, Moyo wangu utafurahi, naam, moyo wangu; Naam, viuno vyangu vitafurahi, Midomo yako inenapo maneno mema. Moyo wako usiwahusudu wenye dhambi; Bali mche BWANA mchana kutwa; Maana bila shaka iko thawabu; Na tumaini lako halitabatilika.
Methali 23:10-18 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani wala kunyemelea kwenye mashamba ya yatima, kwa kuwa Mtetezi wao ni mwenye nguvu, atawatetea dhidi yako. Elekeza moyo wako kwenye mafundisho na masikio yako kwenye maneno ya maarifa. Usimnyime mtoto adhabu, ukimwadhibu kwa fimbo, hatakufa. Mwadhibu kwa fimbo na kuiokoa nafsi yake kutoka mautini. Mwanangu, kama moyo wako una hekima, basi moyo wangu utafurahi, utu wangu wa ndani utafurahi, wakati midomo yako itakapozungumza lililo sawa. Usiuruhusu moyo wako kuwaonea wivu wenye dhambi, bali kila mara uwe na bidii katika kumcha BWANA. Hakika kuna tumaini la baadaye kwa ajili yako, nalo tarajio lako halitakatiliwa mbali.