Mithali 22:7-16
Mithali 22:7-16 NENO
Matajiri huwatawala maskini naye akopaye ni mtumwa wa akopeshaye. Yeye aupandaye uovu huvuna taabu, nayo fimbo ya ghadhabu yake itaangamizwa. Mtu mkarimu yeye mwenyewe atabarikiwa kwa kuwa hushiriki chakula chake na maskini. Mfukuze mwenye dhihaka, na mvutano utatoweka; ugomvi na matukano vitakoma. Yeye apendaye moyo safi na yeye ambaye maneno yake ni ya neema, mfalme atakuwa rafiki yake. Macho ya BWANA hulinda maarifa, bali huyapinga maneno ya asiye mwaminifu. Mvivu husema, “Yuko simba nje!” au, “Nitauawa katika mitaa!” Kinywa cha mwanamke kahaba ni shimo refu; yeye aliye chini ya ghadhabu ya BWANA atatumbukia ndani yake. Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto, bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye. Yeye anayemdhulumu maskini ili kujiongezea mali, naye anayempa tajiri zawadi, wote huwa maskini.