Methali 22:7-16
Methali 22:7-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Tajiri humtawala maskini; mkopaji ni mtumwa wa mkopeshaji. Apandaye dhuluma atavuna janga; uwezo wake wa kutenda mabaya utavunjwa. Mtu mkarimu atabarikiwa, maana chakula chake humgawia maskini. Mfukuze mwenye dharau na fujo itatoweka, ugomvi na matusi vitakoma. Mwenye nia safi na maneno mazuri, atakuwa rafiki wa mfalme. Mwenyezi-Mungu hulinda elimu ya kweli, lakini huyavuruga maneno ya waovu. Mvivu husema, “Siwezi kutoka nje; kuna simba huko, ataniua!” Kinywa cha mwasherati ni shimo refu; anayechukiwa na Mwenyezi-Mungu atatumbukia humo. Mtoto hupenda mambo ya kijinga moyoni, lakini fimbo ya nidhamu humwondolea hayo. Anayemdhulumu maskini atamfanya afaidike mwishowe, anayewapa matajiri zawadi ataishia kuwa maskini.
Methali 22:7-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye. Yeye apandaye uovu atavuna msiba, Na fimbo ya ghadhabu yake itakoma. Mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa; Maana huwapa maskini chakula chake. Mtupe nje mwenye dharau, na ugomvi utatoka; Naam, fitina na fedheha zitakoma. Apendaye usafi wa moyo, na neema ya midomo; Mfalme atakuwa rafiki yake. Macho ya BWANA humhifadhi mwenye maarifa; Bali huyapindua maneno ya mtu haini. Mtu mvivu husema, Simba yuko nje; Nitauawa katika njia kuu. Kinywa cha malaya ni shimo refu; Anayechukiwa na BWANA atatumbukia ndani yake. Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali. Yeye awaoneaye maskini ili kuongeza mapato, Naye ampaye tajiri, hupata hasara.
Methali 22:7-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Methali 22:7-16 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Matajiri huwatawala maskini naye akopaye ni mtumwa wa akopeshaye. Yeye aupandaye uovu huvuna taabu, nayo fimbo ya ghadhabu yake itaangamizwa. Mtu mkarimu yeye mwenyewe atabarikiwa kwa kuwa hushiriki chakula chake na maskini. Mfukuze mwenye dhihaka, na mvutano utatoweka; ugomvi na matukano vitakoma. Yeye apendaye moyo safi na yeye ambaye maneno yake ni ya neema, mfalme atakuwa rafiki yake. Macho ya BWANA hulinda maarifa, bali huyapinga maneno ya asiye mwaminifu. Mvivu husema, “Yuko simba nje!” au, “Nitauawa katika mitaa!” Kinywa cha mwanamke kahaba ni shimo refu; yeye aliye chini ya ghadhabu ya BWANA atatumbukia ndani yake. Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto, bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye. Yeye anayemdhulumu maskini ili kujiongezea mali, naye anayempa tajiri zawadi, wote huwa maskini.