YouVersion Logo
Search Icon

Marko 13:32, 33, 34, 35, 36

Marko 13:32 NENO

“Kwa habari ya siku ile na saa hakuna yeyote ajuaye, hata malaika walio mbinguni wala Mwana, ila Baba peke yake.

Marko 13:33 NENO

Jihadharini! Kesheni! Kwa maana hamjui wakati ule utakapowadia.

Marko 13:34 NENO

Ni kama mtu anayesafiri. Anaiacha nyumba yake na kuwaachia watumishi wake kuiangalia, kila mtu na kazi yake, kisha akamwamuru yule bawabu aliye mlangoni akeshe.

Marko 13:35 NENO

“Basi kesheni, kwa sababu hamjui ni lini mwenye nyumba atakaporudi: iwapo ni jioni, au ni usiku wa manane, au alfajiri awikapo jogoo, au mapambazuko

Marko 13:36 NENO

akija ghafula asije akawakuta mmelala.

Free Reading Plans and Devotionals related to Marko 13:32, 33, 34, 35, 36