Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 29:24-32

Yeremia 29:24-32 NENO

Mwambie Shemaya Mnehelami, “Hili ndilo BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asemalo: Ulituma barua kwa jina lako mwenyewe kwa watu wote wa Yerusalemu, kwa Sefania mwana wa kuhani Maaseya na kwa makuhani wengine wote. Ulimwambia Sefania, ‘BWANA amekuweka wewe uwe kuhani badala ya Yehoyada ili uwe msimamizi wa nyumba ya BWANA. Unapaswa kumfunga kwa mikatale na mnyororo wa shingoni mwendawazimu yeyote anayejifanya nabii. Kwa nini basi hukumkemea Yeremia Mwanathothi, aliyejifanya kama nabii miongoni mwenu? Ametutumia ujumbe huu huku Babeli: Mtakuwa huko muda mrefu. Kwa hiyo jengeni nyumba mkakae; pandeni mashamba na mle mazao yake.’ ” Kuhani Sefania, hata hivyo, akamsomea nabii Yeremia ile barua. Ndipo neno la BWANA likamjia Yeremia kusema: “Tuma ujumbe huu kwa watu wote walio uhamishoni kusema: ‘Hili ndilo asemalo BWANA kuhusu Shemaya Mnehelami: Kwa sababu Shemaya amewatabiria ninyi, hata ingawa sikumtuma, naye amewafanya kuamini uongo, hili ndilo asemalo BWANA: Hakika nitamwadhibu Shemaya Mnehelami pamoja na uzao wake. Hapatakuwa na yeyote atakayebaki miongoni mwa watu hawa, wala hataona mema nitakayowatendea watu wangu, asema BWANA, kwa sababu ametangaza uasi dhidi yangu.’ ”