Yeremia 29:24-32
Yeremia 29:24-32 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu aliniagiza nimwambie hivi Shemaya wa Nehelamu: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Umepeleka barua kwa jina lako kwa wakazi wote wa Yerusalemu na kwa kuhani Sefania mwana wa Maaseya na kwa makuhani wengine wote. Katika barua hiyo, ulimwambia Sefania hivi: ‘Mwenyezi-Mungu amekufanya wewe Sefania kuwa kuhani badala ya kuhani Yehoyada, uwe mkuu wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Ni wajibu wako kumtia gerezani na kumfunga minyororo mwendawazimu yeyote anayetabiri. Kwa nini basi, hukumkemea Yeremia kutoka Anathothi anayekutabiria? Maana yeye alituma taarifa huko Babuloni kwamba uhamisho wenu utakuwa wa muda mrefu, na kusema mjenge nyumba, mkae; mlime mashamba, mpande mbegu na kula mazao yake!’” Kuhani Sefania aliisoma barua hiyo mbele ya nabii Yeremia. Ndipo Mwenyezi-Mungu akamwambia Yeremia: “Wapelekee watu wote walioko uhamishoni ujumbe huu: Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi juu ya Shemaya wa Nehelamu: Shemaya amewatabirieni, hali mimi sikumtuma, akawafanya muuamini uongo. Kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu nasema kuwa nitamwadhibu Shemaya wa Nehelamu pamoja na wazawa wake. Hakuna hata mmoja wa watu wake atakayebaki hai kuona mema nitakayowafanyia watu wangu, kwa sababu amewachochea watu waniasi mimi Mwenyezi-Mungu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Yeremia 29:24-32 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na kuhusu Shemaya, Mnehelami, utanena, ukisema, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, ya kwamba, Kwa kuwa kwa jina lako mwenyewe umewapelekea barua watu wote walioko Yerusalemu, na Sefania, mwana wa Maaseya, kuhani, na makuhani wote, kusema, BWANA amekufanya kuhani badala ya Yehoyada, kuhani, ili mpate kuwa watumishi katika nyumba ya BWANA, kwa kila mtu aliye na wazimu, na kwa kila mtu ajifanyaye kuwa nabii, umtie katika mkatale na pingu. Mbona, basi, hukumkemea Yeremia wa Anathothi, ajifanyaye kuwa nabii kwenu, ambaye ametuma watu kwetu katika Babeli, kusema, Uhamisho huu ni wa siku nyingi; jengeni nyumba, mkakae ndani yake; pandeni bustani, mkale matunda yake. Na Sefania, kuhani, akasoma barua hii masikioni mwa Yeremia nabii. Ndipo neno la BWANA likamjia Yeremia, kusema, Uwapelekee habari watu wote waliohamishwa, kusema, BWANA asema hivi, kuhusu Shemaya, Mnehelami; Kwa sababu Shemaya amewatabiria ninyi, lakini sikumtuma mimi, naye amewatumainisha neno la uongo; basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitamwadhibu Shemaya, Mnehelami, na wazawa wake; hatakuwa na mtu atakayekaa katika watu hawa, wala hatayaona mema nitakayowatendea watu wangu, asema BWANA; kwa sababu amenena maneno ya uasi juu ya BWANA.
Yeremia 29:24-32 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na katika habari za Shemaya, Mnehelami, utanena, ukisema, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, ya kwamba, Kwa kuwa kwa jina lako mwenyewe umewapelekea barua watu wote walioko Yerusalemu, na Sefania, mwana wa Maaseya, kuhani, na makuhani wote, kusema, BWANA amekufanya kuhani badala ya Yehoyada, kuhani, ili mpate kuwa watumishi katika nyumba ya BWANA, kwa kila mtu aliye na wazimu, na kwa kila mtu ajifanyaye kuwa nabii, umtie katika mkatale na pingu. Mbona, basi, hukumkemea Yeremia wa Anathothi, ajifanyaye kuwa nabii kwenu, ambaye ametuma watu kwetu katika Babeli, kusema, Uhamisho huu ni wa siku nyingi; jengeni nyumba, mkakae ndani yake; pandeni bustani, mkale matunda yake. Na Sefania, kuhani, akasoma barua hii masikioni mwa Yeremia nabii. Ndipo neno la BWANA likamjia Yeremia, kusema, Uwapelekee habari watu wote waliohamishwa, kusema, BWANA asema hivi, katika habari za Shemaya, Mnehelami; Kwa sababu Shemaya amewatabiria ninyi, lakini sikumtuma mimi, naye amewatumainisha neno la uongo; basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitamwadhibu Shemaya, Mnehelami, na wazao wake; hatakuwa na mtu atakayekaa katika watu hawa, wala hatayaona mema nitakayowatendea watu wangu, asema BWANA; kwa sababu amenena maneno ya uasi juu ya BWANA.
Yeremia 29:24-32 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mwambie Shemaya Mnehelami, “Hili ndilo BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asemalo: Ulituma barua kwa jina lako mwenyewe kwa watu wote wa Yerusalemu, kwa Sefania mwana wa kuhani Maaseya na kwa makuhani wengine wote. Ulimwambia Sefania, ‘BWANA amekuweka wewe uwe kuhani badala ya Yehoyada ili uwe msimamizi wa nyumba ya BWANA. Unapaswa kumfunga kwa mikatale na mnyororo wa shingoni mwendawazimu yeyote anayejifanya nabii. Kwa nini basi hukumkemea Yeremia Mwanathothi, aliyejifanya kama nabii miongoni mwenu? Ametutumia ujumbe huu huku Babeli: Mtakuwa huko muda mrefu. Kwa hiyo jengeni nyumba mkakae; pandeni mashamba na mle mazao yake.’ ” Kuhani Sefania, hata hivyo, akamsomea nabii Yeremia ile barua. Ndipo neno la BWANA likamjia Yeremia kusema: “Tuma ujumbe huu kwa watu wote walio uhamishoni kusema: ‘Hili ndilo asemalo BWANA kuhusu Shemaya Mnehelami: Kwa sababu Shemaya amewatabiria ninyi, hata ingawa sikumtuma, naye amewafanya kuamini uongo, hili ndilo asemalo BWANA: Hakika nitamwadhibu Shemaya Mnehelami pamoja na uzao wake. Hapatakuwa na yeyote atakayebaki miongoni mwa watu hawa, wala hataona mema nitakayowatendea watu wangu, asema BWANA, kwa sababu ametangaza uasi dhidi yangu.’ ”