1
Mateo 22:37-39
Swahili Roehl Bible 1937
SRB37
Naye akamwambia: Umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa mawazo yako yote! Hili ndilo agizo lililo kubwa, tena ni la kwanza. Nalo la pili limefanana nalo, ndilo hili: Umpende mwenzio, kama unavyojipenda mwenyewe!
Linganisha
Chunguza Mateo 22:37-39
2
Mateo 22:40
Katika haya maagizo mawili yamo Maonyo yote ya Mungu pamoja na Wafumbuaji.
Chunguza Mateo 22:40
3
Mateo 22:14
Kwani waalikwao ni wengi, lakini wachaguliwao ni wachache tu!*
Chunguza Mateo 22:14
4
Mateo 22:30
Kwani katika ufufuko hawataoa, wala hawataolewa, ila watakuwa, kama malaika walivyo mbinguni.
Chunguza Mateo 22:30
5
Mateo 22:19-21
akawauliza: Chapa hiki cha nani? Maandiko nayo ya nani? Wakasema: Ni yake Kaisari. Ndipo, alipowaambia: Basi, yaliyo yake Kaisari mtoleeni Kaisari, naye Mungu yaliyo yake Mungu!
Chunguza Mateo 22:19-21
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video