Naye akawaambia: Ni kwa ajili hammtegemei Mungu vema. Maana nawaambia la kweli: Cheo chenu cha kumtegemea Mungu kikiwa kidogo kama kipunje cha mbegu, mtauambia mlima huu: Ondoka hapa, ulipo, uende pale! nao utaondoka. Hivyo halitakuwako neno lisilowezekana nanyi.