Ndipo, nitakapowakemea walafi kwa ajili yenu, wasiwaangamizie mazao ya nchi, wala mizabibu yenu iliyoko mashambani isikose matunda; ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema. Ndipo, wamizimu wote watakapowatukuza kuwa wenye shangwe, kwani mtakuwa nchi ipendezayo; ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema.