Malaki 3:17-18
Malaki 3:17-18 SRB37
Ndivyo, Bwana Mwenye vikosi asemavyo: Hao watakuwa wangu mimi mwenyewe siku hiyo nitakayoifanya mimi, nami nitawahurumia, kama mtu anavyomhurumia mwanawe aliyemtumikia. Hapo ndipo, mtakapoona tena, ya kuwa wanapambanuka amchaye Bwana naye asiyemcha, tena amtumikiaye Mungu naye asiyemtumikia.