1
Warumi 4:20-21
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
TKU
Hakutilia shaka kuwa Mungu angetenda kile alichoahidi. Hakuacha kuamini. Kwa hakika, aliendelea kuimarika katika imani yake. Alitukuza Mungu na alikuwa na uhakika kuwa Mungu anaweza kutenda alichoahidi.
Linganisha
Chunguza Warumi 4:20-21
2
Warumi 4:17
Kama Maandiko yanavyosema, “Nimekufanya uwe baba wa mataifa mengi.” Abrahamu aliposikia ahadi hii, aliiweka imani yake kwa Mungu. Mungu ndiye awapaye uhai waliokufa na kwa amri yake huumba kisichokuwepo.
Chunguza Warumi 4:17
3
Warumi 4:25
Yesu alitolewa afe kwa ajili ya dhambi zetu, na akafufuliwa kutoka kifo ili Mungu atuhesabie haki.
Chunguza Warumi 4:25
4
Warumi 4:18
Halikuwepo tumaini kwamba Abrahamu angepata watoto, lakini alimwamini Mungu na akaendelea kutumaini. Na ndiyo sababu akafanyika kuwa baba wa mataifa mengi. Kama Mungu alivyomwambia kuwa, “Utakuwa na wazaliwa wengi.”
Chunguza Warumi 4:18
5
Warumi 4:16
Hivyo watu hupokea ahadi ya Mungu kwa imani. Hili hutokea ili ahadi hiyo iwe kipawa cha bure. Na ikiwa ahadi ni kipawa cha bure, basi watu wote wa Abrahamu watapata ahadi hiyo. Ahadi hii si tu kwa ajili ya wale wanaoishi chini ya Sheria ya Musa. Bali ni kwa ajili ya wote wanaoishi kwa kuweka imani yao kwa Mungu kama Abrahamu alivyofanya. Ni baba yetu sote.
Chunguza Warumi 4:16
6
Warumi 4:7-8
“Ni heri kwa watu wanaposamehewa kutokana na mabaya waliyotenda, dhambi zao zinapofutwa! Ni heri kwa watu, Bwana anapozifuta dhambi zao kutoka katika kumbukumbu yake!”
Chunguza Warumi 4:7-8
7
Warumi 4:3
Hili ni wazi kama Maandiko yanavyosema, “Abrahamu alimwamini Mungu, na kwa sababu ya kuamini kwake, Mungu alimhesabu kuwa mwenye haki.”
Chunguza Warumi 4:3