1
Warumi 3:23-24
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
TKU
Ndiyo, watu wote wametenda dhambi na wameshindwa kufikia kiwango cha utukufu wa Mungu kilichokusudiwa kwao. Mungu ameamuru sisi sote tufunguliwe kutoka dhambini. Zawadi hii ya neema yake imekuja kwetu kupitia kile ambacho Kristo Yesu alikifanya ili tuwe huru.
Linganisha
Chunguza Warumi 3:23-24
2
Warumi 3:22
Uaminifu wa wema wa Mungu umedhihirishwa kwetu kupitia imani katika Yesu Kristo. Hufanya hivi kwa wote wanaomwamini Kristo. Kwa sababu kwa Mungu watu wote ni sawa.
Chunguza Warumi 3:22
3
Warumi 3:25-26-25-26
Mungu alimtoa Yesu kama njia ya kusamehe dhambi za watu kupitia imani katika yeye. Mungu anasamehe watu kwa sababu sadaka ya damu ya Yesu iliwaweka huru na dhambi zao. Mungu alimtoa Yesu kuonesha kuwa hutenda haki na bila upendeleo. Alikuwa sahihi huko nyuma alipovumilia na hakuwaadhibu watu kwa sababu ya dhambi zao. Na katika wakati wetu bado anatenda haki. Mungu alifanya hili ili awahukumu watu pasipo kuwa na upendeleo na kumwesabia haki mtu yeyote aliye na imani katika Yesu.
Chunguza Warumi 3:25-26-25-26
4
Warumi 3:20
Kwa sababu kufuata sheria hakumfanyi mtu akahesabiwa haki mbele za Mungu. Sheria inatuonyesha dhambi zetu tu.
Chunguza Warumi 3:20
5
Warumi 3:10-12
Kama Maandiko yanavyosema, “Hakuna atendaye haki, hakuna hata mmoja. Hakuna hata mmoja anayeelewa, hakuna anayetaka kumfuata Mungu. Wote wamegeuka na kumwacha, na hawana manufaa kwa yeyote. Hakuna atendaye mema, hakuna hata mmoja.”
Chunguza Warumi 3:10-12
6
Warumi 3:28
Ninamaanisha kuwa watu hufanyika wenye haki na kukubaliwa na Mungu kwa njia ya imani, siyo kwa sababu ya yale wanayotenda ili kuifuata sheria. Hili ndilo tunaloamini.
Chunguza Warumi 3:28
7
Warumi 3:4
Hapana! Hata ikiwa wengine wote watashindwa kutimiza ahadi zao, daima, Mungu atatekeleza aliyosema. Kama Maandiko yanavyosema kuhusu Mungu, “Utathibitika kuwa mwenye haki kwa maneno yako, na utashinda utakaposhitakiwa na watu.”
Chunguza Warumi 3:4