“Je, huko kuongeza idadi ya mierezi
kutakufanya uwe mfalme?
Je, baba yako hakula na kunywa?
Alifanya yaliyo sawa na haki,
naye akafanikiwa kwa yote.
Aliwatetea maskini na wahitaji,
hivyo yeye akafanikiwa katika yote.
Je, hiyo si ndiyo maana ya kunijua mimi?”
asema BWANA.