YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 50

50
Ibada ya kweli
(Zaburi ya Asafu)
1Mungu wa nguvu#50:1 Mungu wa nguvu: Hivyo, kadiri ya makala ya Kiebrania; au Mungu Mkuu. Mwenyezi-Mungu, amenena,
amewaita wakazi wa dunia,
tokea mawio ya jua hadi machweo yake.
2Kutoka Siyoni, mji mzuri mno,
Mungu anajitokeza, akiangaza.
3Mungu wetu anakuja, na sio kimyakimya:
Moto uunguzao wamtangulia,
na dhoruba kali yamzunguka.
4Kutoka juu anaziita mbingu na dunia;
zishuhudie akiwahukumu watu wake:
5“Nikusanyieni waaminifu wangu,
waliofanya agano nami kwa tambiko!”
6Mbingu zatangaza uadilifu wa Mungu;
kwamba Mungu mwenyewe ni hakimu.
7“Sikilizeni watu wangu, ninachosema!
Israeli, natoa ushahidi dhidi yako.
Mimi ni Mungu! Mimi ni Mungu wako!
8Sikukaripii kwa sababu ya tambiko zako;
hujaacha kunitolea tambiko za kuteketeza.
9Kwa kweli sina haja na fahali wa zizi lako,
wala beberu wa mifugo yako;
10maana wanyama wote porini ni mali yangu,
na maelfu ya wanyama milimani ni wangu.
11Ndege wote wa mwitu ni mali yangu,
na viumbe vyote hai mashambani ni vyangu.
12Kama ningeona njaa singekuambia wewe,
maana ulimwengu na vyote vilivyomo ni vyangu.
13Je, wadhani nala nyama ya fahali,
au Kunywa damu ya mbuzi?
14Shukrani iwe ndio tambiko yako kwa Mungu
mtimizie Mungu Aliye Juu ahadi zako.
15Uniite wakati wa taabu,
nami nitakuokoa, nawe utaniheshimu.”
16Lakini Mungu amwambia mtu mwovu:
“Ya nini kuzitajataja tu sheria zangu?
Kwa nini unasemasema juu ya agano langu?
17Wewe wachukia kuwa na nidhamu,
na maneno yangu hupendi kuyafuata.
18Ukimwona mwizi unaandamana naye,
na wazinzi unashirikiana nao.
19Uko tayari daima kunena mabaya;
kazi ya ulimi wako ni kutunga uongo.
20Wakaa kitako kumsengenya binadamu mwenzako,
naam, kumchongea ndugu yako mwenyewe.
21Umefanya hayo yote nami nimenyamaa.
Je, wadhani kweli mimi ni kama wewe?
Lakini sasa ninakukaripia,
ninakugombeza waziwazi.
22“Fikirini vizuri jambo hili, enyi msionijali,
la sivyo nitawaangamizeni,
wala hapatakuwa na wa kuwaokoeni.
23Anayenipa shukrani kama tambiko yake,
huyo ndiye anayeniheshimu;
yeyote anayedumu katika njia yangu,
huyo ndiye nitakayemwokoa.”

Currently Selected:

Zaburi 50: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy