Zaburi 135:6-12
Zaburi 135:6-12 BHN
Mwenyezi-Mungu hufanya chochote anachotaka, mbinguni, duniani, baharini na vilindini. Ndiye aletaye mawingu kutoka mipaka ya dunia; afanyaye gharika kuu kwa umeme, na kuvumisha upepo kutoka ghala zake. Ndiye aliyewaua wazaliwa wa kwanza huko Misri, wazaliwa wa watu na wanyama kadhalika. Ndiye aliyefanya ishara na maajabu kwako, ee Misri, dhidi ya Farao na maofisa wake wote. Ndiye aliyeyaangamiza mataifa mengi, akawaua wafalme wenye nguvu: Kina Sihoni mfalme wa Waamori, Ogu mfalme wa Bashani, na wafalme wote wa Kanaani. Alichukua nchi zao na kuwapa watu wake; naam, ziwe riziki ya watu wake Israeli.