Zaburi 63
63
Hamu ya kuwa pamoja na Mungu
1Zaburi ya Daudi wakati alipokuwa katika jangwa la Yudea.
2Ee Mungu,
wewe ni Mungu wangu.
Moyo wangu unakutafuta,
roho yangu inasikia kiu yako,
ninasikia kiu yako kama inchi inayokauka kwa ukosefu wa maji.
3Nina hamu ya kukuona katika pahali pako patakatifu,
nione nguvu yako na utukufu wako.
4Wema wako ni bora kuliko maisha.
Nitakusifu kwa midomo yangu.
5Nitakushukuru maisha yangu yote,
nitakuomba nikikuinulia mikono yangu.
6Roho yangu itafurahi kama mwenye kushiba minofu yenye mafuta,
kwa shangwe nitaimba sifa zako.
7Ninakukumbuka ninapokuwa katika kitanda,
ninafikiri juu yako usiku kucha,
8maana wewe umenisaidia siku zote.
Nitashangilia chini ya kivuli cha mabawa yako.
9Roho yangu inashikamana nawe kabisa;
unanilinda kwa mukono wako wa kuume.
10Lakini hao wanaokusudia kupoteza maisha yangu,
watatumbukia chini kwenye makao ya wafu.
11Watauawa kwa upanga,
maiti zao zikuwe chakula cha mbweha.
12Lakini mufalme atamufurahia Mungu;
nao wote wanaoapa kwa jina la Mungu watamusifu,
lakini vinywa vya waongo vitafungwa.
Currently Selected:
Zaburi 63: SWC02
Highlight
Copy
Compare
Share
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

:
Highlight
Copy
Compare
Share
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.