Zaburi 144
144
Shukrani kwa ajili ya ushindi
1Zaburi ya Daudi.
Atukuzwe Yawe, yeye ni:
nguvu yangu,
yule anayeizoeza mikono yangu kupigana vita na kuvifundisha vidole vyangu kugombana,
2rafiki yangu wa kweli,
kimbilio langu,
upango wangu,
mukombozi wangu,
ngao yangu,
yule anayenilinda,
yule anayeshinda mataifa na kuyaweka chini yangu.
3Ee Yawe, mutu ni nini hata umujali?
Mwanadamu ni nini hata ufikiri juu yake? #Ang. Zab 8.4
4Mwanadamu ni kama pumzi tu;
siku zake zinapita kama kivuli.
5Uinamishe mbingu zako, ee Yawe, ushuke chini!
Uiguse milima, nayo itoe moshi!
6Upige umeme, uwasambaze waadui;
upige mishale yako, uwakimbize!
7Unyooshe mukono wako kutoka juu,
uniopoe katika maji haya mengi,
uniokoe kutoka makucha ya wageni
8ambao wanasema maneno ya uongo
na kunyoosha mukono kwa kushuhudia uongo.
9Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mupya;
nitakupigia kinubi cha nyuzi kumi,
10wewe unayewapa wafalme ushindi,
unayemwokoa mutumishi wako Daudi!
11Uniokoe kutoka upanga wa waadui wakali,
uniokoe kutoka makucha ya wageni,
ambao wanasema maneno ya uongo,
wanaonyoosha mukono kwa kushuhudia uongo.
12Katika ujana wao, wana wetu wakuwe kama mimea iliyostawi vizuri;
nao wabinti wetu wakuwe wazuri kama nguzo zilizochongwa kwa kupamba nyumba ya kifalme.
13Gala zetu zijae mavuno ya kila aina.
Kondoo wetu katika mbuga wazae maelfu na maelfu.
14Ngombe wetu wakuwe na afya na nguvu,
kusitokwe mimba wala kukosa kuibeba.
Kusikuwe tena kilio katika mitaa yetu.
15Heri taifa ambalo limejaliwa hayo!
Heri taifa ambalo Yawe ndiye Mungu wao!
Currently Selected:
Zaburi 144: SWC02
Highlight
Copy
Compare
Share
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

:
Highlight
Copy
Compare
Share
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.