Bible App logo
Search Icon

Zaburi 138

138
Maombi ya shukrani
1Zaburi ya Daudi.
Ninakushukuru, ee Yawe, kwa moyo wangu wote,
ninaimba sifa zako mbele ya miungu.
2Ninainama uso mpaka chini
kuelekea hekalu lako takatifu.
Ninalisifu jina lako,
kwa sababu ya wema na uaminifu wako.
Umeheshimisha jina lako na neno lako
kuliko vitu vyote.
3Nilipokulilia, wewe ulinijibu;
umeniongezea nguvu yangu.
4Wafalme wote katika dunia watakusifu, ee Yawe,
kwa sababu wameyasikia maneno yako.
5Wataimba sifa za matendo yako, ee Yawe,
kwa maana utukufu wako ni mukubwa.
6Ee Yawe, ingawa wewe uko juu ya wote,
unawaangalia wanyenyekevu kwa wema;
lakini, unatambua wenye kiburi kwa mbali.
7Hata nikisongwa na taabu, wewe unanilinda.
Unanyoosha mukono wako juu ya waadui zangu wakali,
kwa nguvu yako kubwa unaniokoa.
8Ee Yawe, utatimiza yote uliyoniahidia.
Wema wako, ee Yawe, unadumu milele.
Usisahau kazi ya mukono wako mwenyewe.

Currently Selected:

Zaburi 138: SWC02

Highlight

Copy

Compare

Share

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in