Zaburi 130
130
Kuomba musaada
1Wimbo wa safari za kidini.
Tokea humu katika taabu inayonilemea,
ninakulilia, ee Yawe.
2Ee Bwana, usikie sauti yangu,
ulitegee ombi langu sikio.
3Ee Yawe, kama ungekumbuka maovu yetu,
nani, ee Bwana wetu, angeweza kuishi?
4Lakini kwako tunapata usamehe,
kusudi sisi tukuheshimu.
5Ninamutumainia Yawe kwa moyo wangu wote.
Ninaaminia sana neno lake.
6Ninamungojea Yawe
kuliko vile wazamu wanavyongojea mapambazuko,
ndiyo, kuliko vile wazamu wanavyongojea mapambazuko.
7Ee Israeli, umutumainie Yawe,
maana Yawe ni mwenye wema,
naye ana nguvu kubwa ya kutukomboa.
8Yeye atawakomboa watu wa Israeli
kutoka katika maovu yao yote. #Ang. Mat 1.21; Tito 2.14
Currently Selected:
Zaburi 130: SWC02
Highlight
Copy
Compare
Share
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.