Bible App logo
Search Icon

Zaburi 123

123
Kuomba huruma
1Wimbo wa safari za kidini.
Ninainua macho kwako, ee Yawe,
wewe unayeikaa huko juu mbinguni!
2Kama watumishi wanavyomutegemea bwana wao,
kama mujakazi anavyomutegemea bibi mukubwa wake,
ndivyo nasi tunavyokutegemea wewe,
ee Yawe, Mungu wetu,
mpaka hapo utakapotuonea huruma.
3Utuhurumie, ee Yawe, utuhurumie,
maana tumezarauliwa kupita kipimo.
4Tumeshiba muda murefu mazarau ya watajiri,
nayo masimango ya wenye kiburi.

Currently Selected:

Zaburi 123: SWC02

Highlight

Copy

Compare

Share

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in