Zaburi 110
110
Kusimikwa kwa mufalme muchaguliwa
1Zaburi ya Daudi.
Yawe anamwambia bwana wangu:
“Ikaa na mamlaka kwa kuume kwangu
mpaka nitakapowaweka waadui zako chini ya miguu yako.”#Ang. Mat 22.44; Mk 12.36; Lk 20.42-43; Mdo 2.34-35; 1 Kor 15.25; Efe 1.20-22; Kol 3.1; Ebr 1.3; 8.1; 10.12-13
2Yawe ataeneza mamlaka yako kutoka Sayuni;
utatawala juu ya waadui zako wote.
3Watu wako watajitolea,
siku utakapokwenda kuwapiga waadui.
Juu ya milima mitakatifu vijana wako watakufikia,
kama umande unaotokeza asubui mapema.#110.3 au: “Kwako ni cheo cha kifalme tangu ulipozaliwa juu ya milima mitakatifu. Kutoka ndani ya tumbo, mbele ya mapambazuko, nilikuzaa.”
4Yawe amekuapia hivi wala hatabadilisha nia yake:
“Wewe ni kuhani milele kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.” #Ang. Ebr 5.6; 7.17,21
5Bwana wetu yuko karibu nawe;
atawaponda wafalme atakapokasirika.
6Atayahukumu mataifa na kuwaua watu wengi;
atawaponda waongozi kila nafasi katika dunia.
7Mufalme atakunywa maji ya kijito katika njia,
kisha atainua kichwa kwa ushindi.
Currently Selected:
Zaburi 110: SWC02
Highlight
Copy
Compare
Share
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.